Manispaa ya Sumbawanga kupitia mradi wa uboreshsaji miji imetenga kiasi cha shilingi 7,368,573,061 kwaajili ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 4.6 itakayounganisha kata za Majengo, Msua na Chanji.
Mradi huo ulioanza mwishoni mwa mwaka 2017 tayari umeshatumia shilingi bilioni 1.6 na kutegemewa kumalizika mwezi wa 9 mwaka 2018 inayotoka Mwaiseni, kata ya chanji kupitia Johnkella, kata ya Msua hadi Kanisa la Neema katika kata ya Majengo.
Katika kuuelezea mradi huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu amesema kuwa ukamilifu wa ujenzi huo utapunguza uharibifu wa vyombo usafiri na kuboresha muonekano wa mji wa Sumbawanga.
“Hadi kufikia mwisho wa mwaka tunaamini barabara hii itakuwa imekamilika kulingana na mkataba uliopo na kutoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi na wafanyabiashara katika Mji wa Sumbawanga,” Amesema.
Ujenzi wa barabara hiyo utachochea shughuli za kiuchumi, ajira na kipato katika Manispaa ya Sumbawanga na kupunguza msongamano katikati ya mji.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa