Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu amesema kuviwezesha vikundi vya ujasiliamali ni kuzalisha ajira na ubunifu kwa vijana na wanawake hao ambao ndio nguzo ya maendeleo ya mji wa Sumbawanga nan chi kwa ujumla.
Ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi hundi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milini 20 kwa vikundi 13 vya wanawake, vikundi 3 vya vijana na kimoja cha walemavu katika mkutano mfupi uliuofanyika katika ukumbi wa manispaa hiyo mapema mwezi huu.
Amesema “Nia ya manispaa yetu ni kuongeza kipato kwa wanakikundi, kuinua hali ya maisha yao, kuboresha hali ya maisha ya kiuchumi ngazi ya kaya pamoja na kuboresha maisha ya wajasiliamali.”
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa