Tatizo la wauza viatu wa soko la Mandela mjini Sumbawanga kukosa eneo la kufanyia biashara zao limetatuliwa na uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga.
Awali Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr.Halfan Haule aliuagiza uongozi wa Manispaa kutowahamisha wafanyabiashara hao wa kuuza viatu kwenye eneo la stendi za Daladala za Mandela hadi pale watakapo watafutia eneo jingine tofauti na hilo ambalo litakuwa rafiki kwa biashara yao.
Kufuatia agizo hilo uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw.Saad Mtambule aliitisha kikao cha pamoja baina ya wafanyabiashara hao wa viatu na viongozi wa chama cha Madereva Daladala ambao kwa kauli moja wafanyabishara wa viatu walikubali kuondoka eneo hilo na kukubali kuhamia eneo jipya waliloelekezwa na Manispaa umbali wa takribani mita 100 toka walipokuwa awali ambapo wanaamini patakuwa ni eneo rafiki kwa wateja wao na biashara pia.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa