Watendaji wa Ofisi ya Elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Wakuu wa Shule za Sekondari sanjari na Walimu Wakuu wa wameshauriwa kujenga ushirikiano imara ili kuweza kutatua nchangamoto balimbali za elimu kwenye halmashauri hiyo.
Kutolewa kwa kauli hiyo kumeambatana na Uzinduzi wa Miongozo ya Elimu kwa Manispaa hiyo yenye lengo la kuboresha utendaji kazi kwa shule zote za Manispaa ya Sumbawanga.
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba alisema zipo changamoto nyingi kwenye shule hizo ambazo zinaathiri ufundishaji lakini zinaweza kumalizwa kwa kushariana kati aya Wataalkamu wa elimu na viongozi wanaoziongozo shule hizo.
Waryuba alisema kuwa ufanisi wa kazi kwenye shule zote za Sekondari na Shule za Msingi, unatatokana na uteuzi mzuri wa Wakuu wa Shule na Wlimu wakuu ambao wanahekima za uongozi na walioteuliwa kwa kufuata maadili bora ya uongozi na sio vinginevyo/
Aidha aliwataka Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule kushirikiana vyema na Walimu wao kwa kutatua changamoto zao kwa lengo la kuwawezesha kufanya kazi kwa uhuru huku wakiwekeza akili yao katika kuwafundisha wanafunzi wao.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa