Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imefanikiwa kuongeza kiwango cha vijiji ambavyo vinapata maji ya bomba kutokana kupanuka kwa huduma hiyo kwenye vijiji mbalimbali ikiwa ni matunda ya miradi ya maji ya hivi karibuni na ya muda mrefu.
Mhandisi wa maji katika Manispaa ya Sumbawanga Mhandisi Kazoya Mong’ateko amesema ongezeko la wananchi wanaotumia maji limeongezeka kutoka asilimia 50 hadi 60.
Mhandishi Mong’ateko alisema kukamilika kwa miradi hiyo kumeongezeka huku kukiwa na vituo 64 vya kuteka maji hadi kufika vituo 424.
Alisema hivi karibuni Manispaa ya Sumbawanga imekamilisha na miradi ya maji ya mwaka 2017/18 katika mtandao wa bomba kwenye vijiji vya Kasense, Chipu, Matanga na Kisumba ambapo katika miradi hiyo jumla ya Lita 315,000 zinapatakana kila siku, huku ikifanikiwa kujenga tanki kubwa la maji katika eneo la Mtipe ambalo linakusanya maji kutoka chanzo cha Salumbwa- Chelenganya-Mtipe.
Aidha alidai kuwa katika miradi hiyo ya maji halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imefanikiwa kutatua matatizo ya wananchi kutembea umbali mrefu kusaka maji, sanjari na kupata magonjwa ya homa za matumbo katika vijiji hivyo.
Mhandishi Mong’ateko alisema bado Manispaa ya Sumbawanga inaendelea kuweka mikakati ya miradi mipya ya maji katika vijiji ambavyo bado havina maji ya bomba na kuongeza kuwa katika mwaka ujao wa fedha wanatarajia kujenga miradi hiyo kwenye vijiji vya Katumba Azimio, Mawenzusi, Mponda na Mtimbwa.
Pamoja na hayo ametoa wito kwa wanachi hao kuitunza miradi hiyo ya maji kwa kuvitunza vyanzo vya maji na miundombinu yake.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa