Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeanza mkakati wa urasimishaji wa makazi holela ya wakazi wa mji huo waliojenga kiholela, huku ikiazimia kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote atakayejenga nyumba pasipo kibali cha ujenzi kuanzia hivi sasa.
Hatua hiyo inafuatia kuongezeka kwa kasi ujenzi wa nyumba katika mji wa Sumbawanga huku wamiliki wa nyumba hizo wakijenga pasipo kuwasiliana na Idara ya mipango miji katika Manispaa hiyo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Bw.Jacob Ntalitinya alisema mkakati huo utaanza kwa kuzitambua nyumba zote zilizojengwa pasipo kibali.
Ntalitinya alisema zoezi hilo limeanza kwa kuwatangazia wananchi hao kasha itafuata kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kutambuliwa kwa makazi yao, ambapo watatakiwa kulipia gharama kidogo ili wapate leseni na baadaye hati za nyumba zao.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuanzia sasa hawatataka kuona mtu yeyote ambaye atajenga pasipo kibali cha ujenzi kutoka idara ya Mipango miji.
“Hii ni Manispaa na unapotaka kujenga ni lazima ufuate taratibu na sheria zilizowekwa na sio kufanya mambo kiholela”.alisema Ntalitinya.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa