Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imetoa mafunzo kwa waheshimiwa madiwani na viongozi wa serikli za vijiji 12 katika kata 6 za Manispaa ili ili kuwajulisha namna ya kuunda na kusajili vyombo vya watumia maji vijijini.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu ameeleza kuwa lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo viongozi kuwashirikisha wananchi kwenye miradi maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji.
“Lengo kuu la semina hii viongozi wakahamasishe jamii husika juu ya namna ya kusimamia miundombinu na rasilimali za maji pamoja na kuwa wa kwanza kuwakataza wananchi wanaoendeleza shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji,” Njovu alisema.
Mafunzo hayo ambayo yameendeshwa na idara ya maji ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kufuata Sera ya maji yam waka 2002 na sheria namba 11 ya mwaka 2009 ya usimamizi wa rasilimaji za maji ambazo inazitaka halmashauri kuunda jumuiya za watumiaji maji vijijini ili kuweza kujisimamia na kuendeleza miradi ya maji.
Aidha, Serikali imekuwa ikielekeza nguvu nyingi katika kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji vijijini lakini imekuwa ikikosa usimamizi wa karibu kutokana na jamii husika kutoshiriki kikamilifu kuitunza miradi hiyo. Hivyo jamii imetakiwa iione miradi hiyo ni mali yao na ni jukumu lao kuilinda na kuisimamia kikamilifu ili kuendeleza kutoa huduma bora.
Mafunzo hayo yaliyojumuisha madiwani, Watendaji wa kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti pamoja na viongozi wa jumuiya za watumiaji maji vijiji (COWSO), wameweza kuelezwa mada mbalimbali ikiwemo Dhana ya jamii kumiliki na kusimamia miradi, huduma bora kwa mteja katika miradi ya maji, usimamizi wa fedha za maji, uendeshaji na matengenezo, mpango wa maji salama, na uundaji na usajili wa COWSO.
Mradi huu umelenga kuvifikia vijiji 17 ambapo miradi hiyo itaendeshwa kwa awamu na kila awamu itakuwa ikichukua vijiji vinne amabapo mpaka sasa Kijiji cha Chelenganya, Malonje, Malagano na Tamasenga tayari wameshafikiwa na miradi hiyo kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 na kwa mwaka wa fedha 2016/2017 miradi hiyo inaendelea katika vijiji vya Kasense, Chipu, Matanga na Kisumba na kwa mwaka wa fedha 2017/2018 vijiji vya Mawenzusi, Nambogo, Katumba Azimio na Mponda ndivyo vitakavyofaidika.
Nae Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Sumbawaga Kazoya Mong’ateko ameongeza kuwa mafunzo hayo yametolewa ili kwa wale ambao hawajafikiwa na mradi wawe tayari pindi watakapofikiwa na mradi huo na kuongeza kuwa maandalizi na elimu kwa wananchi ni muhimu ili wananchi hao wawe tayari kuipokea miradi hiyo pindi bajeti itakaporuhusu.
“Tunawapa mafunzo haya ili muwe tayari pindi mradi itakapokuwa imewafikia, lakini pia ni vizuri kuendelea kuvitunza vyanzo vya maji kabla miradi hiyo haijawafikia na pia kitendo cha wananchi kuata mabomba ni kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maenedeleo,” Kazoya alisema.
Nae mwanasheria wa Manispaa ya Sumbawanga James Makwinya aliwakaribisha wananchi hao waweze kufika ofisini kwakwe kwa utaratibu wa kuandaa katiba za jumuia hizo ili kuwarahishia na kuweza kusajiliwa kwa jumuia hizo.
Akifunga mafunzo hayo Mstahiki Meya wa manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa nae alisisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji kwa lengo la kuipusha manispaa kuwa jangwa na kuwasihi viongozi kutokata tamaa na kuwa miongoni mwa watu wanaowakatisha tamaa wananchi wao wanaowaongoza na hatimae wananchi kutotii maagizo ya serikali.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa