Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameishauri Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga kuanza kufikiria kuwa na kiwanda cha viatu vya Ngozi ili kupunguza idadi ya viwanda 25 vipya walivyoagizwa kuwa navyo hadi kufikia Disemba 2018.
Mh. Wangabo ametoa ushauri huo baada ya kutembelea machinjio ya manispaa hiyo na kuona mzigo wa Ngozi za ng’ombe ukiwa umekosa soko na kuongeza kuwa soko la Ngozi hizo litaopatikana pale tu kiwanda kitakapooanza kufanya kazi na kuhakikisha wanashirikiana na shule kwaajili ya soko la viatu hivyo.
“Ngozi tunayo ndiyo malighafi, kiwanda kikowapi ili hii malighafi itumike, tuweke nguvu kubwa hapa kuanzisha kiwanda, Manispaa mna viwanda 25 mnatakiwa kuvianzisha hadi kufikia Disemba 2018, ikiwezekana mshirikiane na SIDO na wale wote wenye viwanda vidogo vinavyotumia malighafi ya Ngozi muwawezeshe ili tuweze kupanuka,” Alifafanua.
Machinjio hayo ambayo tangu mwezi July hadi Novemba 2017 wamechinja ng’ombe 3,807, mbuzi 1,211 na kondoo 98 na kuzalisha Ngozi zaidi ya 10,000 katika miezi 6 jambo linalowawezesha kuanzisha kiwanda kidogo kinakachopunguza idadi ya viwanda 25 walivyotakiwa kuanzisha kabla ya Disemba, 2018.
Nae Nae Afisa mifugo wa Manispaa ya Sumbawanga Nziku amesema kuwa machinjio hiyo ina uwezo wa kuchinja ng’ombe 50 na mbuzi na kondoo 10 kwa wakati mmoja lakini kwasasa inachinja ng’ombe 25 -30 na mbuzi na kondoo 5 – 10 kwa siku.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa