Wajumbe wa serikali za Mitaa ALAT mkoani Rukwa wameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kutumia vyema kiasi cha Shilingi Milioni Mia Tano kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la Wodi ya wazazi ( Mama na Mtoto) lililojengwa katika eneo kituo cha Afya Mazwi.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzake, Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mh.Kalolo Ntila alisema wao kama timu wametembelea mradi huo na wameridhishwa na kufurahishwa mno na namna ya kituo hicho kilivyojengwa.
Mh.Ntila alisema wataalamu wa wametumia vizuri fedha zilizotengwa na kuongeza kuwa hata ramani yake ya jengo hilo ni ya kisasa ambapo wajawazito na wataoto wachanga watakaozaliwa watakuwa katika mazingira salama na bora.
“Tunajua kuwa mmejenga kwa mtindo wa ‘Force Account’ lakini mnahitaji kupongezwa kwa namna mlivyolipangilia hili jengo kiujumla linavutia sana, nawapongeza sana na naomba ikiwezekana halmashauri zingine zije kujifunza kwenu’’.
Hatahivyo wametoa maelekezo kwa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wanakamilisha jengo hilo kwa haraka ikiwa ni pamoja na kumalizia mambo madogo madogo yaliyosalia ili huduma iweze kuanza mara moja.
Kwa upande wake Kaimu Mhandisi wa ujenzi wa Manispaa ya Sumbawanga John Myovela alisema jumla ya Shilingi Milioni 504 zimetumika hadi sasa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo na bado kiasi kidogo cha fedha kinahitajika kumalizia kazi ndogo kwa mafundi, japokuwa vifaa vyote vya kukamilisha kazi hiyo viko tayari.
Kukamilika kwa jengo hilo na kuanza kutoa huduma kutaondoa msangamano wa wajawazito wanaokwenda kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa