Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeanza kutekeleza mradi wa uboreshaji na Uimarishaji Miji, Manispaa na Majiji kwa kujenga kilometa 14 za lami kwa barabara za katikati yaa mji zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 21 ikiwa ni mradi unaotekelezwa na serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
Mradi unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 ambapo Mkandarasi kutoka Kampuni GEO Engineering amekabidhiwa rasmi kuanza kazi hiyo.
Mratibu wa mradi huo wa TACTICS Mhandisi John Myovela amesema kuwa utekelezwaji wa mradi utakwenda sanjari na ujenzi wa Soko la mazao katika eneo la Kanondo ambapo kwa pamoja unatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni 29.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Catherine Mashalla licha ya kufurahia kupokea kwa miradi hiyo aliipongeza serikali ya awamu ya Sita kwa kuridhia kutoa fedha za miradi ya TACTICS katika mji wa Sumbawanga.
Mashalla alisema Manispaa yake imekuwa miongoni mwa halmashari 12 za awali ambazo zimepata bahati ya kuanza kutekeleza miradi hiyo kati ya halmashauri 45 za Miji, Manispaa na Majiji hapa nchini zinazopata fursa hiyo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa