By Kisika S- Kitengo cha Mawasiliano SMC
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeanza mikakati ya kuanzisha viwanda ili kuongeza wigo wa mapato wa halmashauri hiyo.
Mikakati hiyo ya halmashauri imebainishwa kwenye kikao cha Nnne cha Baraza la Madiwani.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Pendo Mangali alisema kuwa wamepokea maoni ya wadau wengi ambao wamekuwa wakiishauri halmashauri hiyo kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato ya ndani kwa kuanzisha vyanzo vipya vya kodi.. alisems Mangali.
‘Nilipokuwa halmashauri ya Siha nilianzisha viwanda viwili kule na ikawa ni moja ya halmashauri ya mfano hapa nchini kwa kuwa na viwanda, hivyo sinabudi kuhamishia wazo hilo kwenye Manispaa hii”
“Wazo la kuendeleza kiwanda cha kutengeneza tofali pasipo kujali ushindani wa soko uliopo kwasababu kila mtu ana fursa yake katika soko la bidhaa yake”, ni kauli ya Mkurugenzi huyo akizungumzia kiwanda cha tofali cha halmashauri hiyo kilichofungwa kwa sasa.
‘Nilipokuwa halmashauri ya Siha nilianzisha viwanda viwili kule na ikawa ni moja ya halmashauri ya mfano hapa nchini kwa kuwa na viwanda, hivyo sinabudi kuhamishia wazo hilo kwenye Manispaa hii”
Aliongeza kuwa kinachotakiwa ni kuthubutu kufanya ili tija ionekana katika viwanda vitakavyoanzishwa kwani licha ya kuongeza mapato pia itatoa ajira kwa makundi mbalimbali hususan ni vijana.
Katika mwaka wa fedha wa 2023/24, halmashauri ya Manispaa ilikusanya mapato ya ndani kiasi cha Sh. 3.02 Bilioni ikiwa imefanikiwa kuvuka lengo kwa asilimia 110.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa