Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa wameishukuru serikali kupitia mradi wa P3 kwa kuwapa mafunzo ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma ambayo yamewapa uelewa mkubwa kiuongozi.
Akizungumza kwa niaba yao Mwenyekiti wa Madiwani hao katika mafunzo hayo Vitalis Ulaya alisema licha mafunzo hayo kuchelewa kutolewa kwao tangia wachaguliwe mwaka Oktoba 2015 lakini yamewasaidia sana kuweza kujenga mkakati wa pamoja katika kuongoza kata zao na hata kujenga mahusiano mazuri baaina yao na Watendaji wa halmashauri zao.
"Walimu wetu kutoka chuo cha Serikali za Mitaa cha Homboro wametusaidia sana kutupa maarifa ya uongozi na tunauhakiki sasa mambo yatakwenda vizuri kwani ilie migongano isiyo yalazima katika halmashauri zetu,"
Aidha aliishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa mafunzo hayo na kuongeza kuwa iendelee kuwapa maarifa kila inapopata fursa ya aina hiyo huko mbeleni.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga yakiwa yameratibiwa na mradi wa P3 chini ya Ufadhili wa serikali ya Amerika (USAID).
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa