Madiwani mkoani Rukwa wametakiwa kutumia nafasi zao kisiasa kwa kuwaadhibu Watendaji wa halmashauri zao ambao wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya kuhujumu mapato ya halmashauri hizo.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Stephene Zelote wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma katika mradi wa P3 yakifadhiliwa na serikali ya Amerika yanayofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Zelote alisema ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na utekelezaji wa miradi ya maendeleo imekuwa ya kusuasua kutokana na uzembe na ubadhirifu wa baadhi ya watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakifanya vitendo viovu vya ufujaji kwa manufaa yao binafsi.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliwatahadharisha Madiwani wa halmashauri zote za mkoa wa Rukwa kutotumia nafasi zao za kisiasa kwaajili ya kupata zabuni katika halmashauri zao kwani kufanya hivyo kutochochea utendaji mbovu wa halmashauri zao.
Aliwataka kuhakikisha wanasimamia huduma bora kwa wananchi wao hadi ngazi za chini lakini pia wakiwapa nafasi wananchi kuzungumza kero zao zinawakabili na zitatuliwe kwa haraka.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa