Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu amewataka wakuu wa idara kutochoka kutoa miongozo kwa watumishi wapya wanaoajiriwa serikalini ili waendane na taratibu za kimaadili ya kazi wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku kwenye maeneo yao ya kazi.
Ameyazungumza hayo alipokuwa akifungua kikao cha mafunzo ya kiongozi cha utaratibu wa mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya wa Sekretarieti za mikoa na mamalaka za serikali za mitaa yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Rais – Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) na mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
Pia alitumia nafasi hiyo kuishukuru idara ya utumishi ya Manispaa kwa kuweza kuendesha mafunzo kwa watumishi wapya na kuwaomba hayo watakayoyapata kutokana na mafunzo hayo yanayoendelea pia wayafikishe kwa watumishi hao.
Mafunzo hayo ambayo yanajumuisha wakuu wa idara ni maalum kwaajili ya kuwaongezea uelewa wakuu hao ili kuimarisha utendaji kazi wao pamoja na watu wanaowaongoza kwenye idara zao ili kuwa na utendaji mzuri unaozingatia maadili katika kazi.
Aidha, alitoa shukurani kwa mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa kuwezesha kufanikisha zoezi hilo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa