Anaandika Sammy Kisika.
Halmasahauri ya Manispaa ya Sumbawanga imepeleka maombi maalumu serikali ya kuomba kuajiri watumishi wa idara ya afya zaidi ya 200, ili kuweza kutoa huduma kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali ya wilaya.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Sebastian Siwale amesema mahitaji ya watumishi hao yanatokana na fedha nyingi zilizotolewa na serikali kwaajili zahanati nne zilizokamilishwa ujenzi wake, huku vituo vya Afya viwili vikajengwa kwenye kata zilizopo nje ya mji na hospitali ya wilaya ya Manispaa hiyo iliyojengwa eneo la Isofu.
Dk. Siwale alizitaja zahanati zilikouwa zimejengwa kufikia hatua ya mamboma kisha serikali ikatoa fedha za kumaliziwa ni pamoja na ile ya kijiji cha Kankwale, Mponda, Nambogo na Fyengeleza.
Wakati vituo vya Afya vinavyoendelea kujengwa ni kile cha Kata ya Mollo na Matanga ambapo vyote kwa pamoja serikali imetoa takribani shiilingi Bilioni moja kujenga vituo hivyo.
Mganga huyo amesema serikali inaendelea kuiboresha sekta ya afya katika Manispaa hiyo ambapo fedha nyingi zimetolewa kwa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kukamilisha ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Isofu na nyongeza ya Shilingi Milioni 300 kwaajili kuanza kununua vifaa tiba ili huduma zianze kutolewa wakati wakisubiri fedha za ujenzi wa wodi za wajawazito na watoto katika hospitali hiyo.
Alisema kupatika na kwa fedha hizo ni hatua kubwa ya mafanikio kwa halmashauri hiyo ambayo huduma za afya zinazidi kuboreshwa tofauti na siku za nyuma.
“Kwa kweli tunampongeza sana Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan, kwasababu hivi sasa maeneo mengi ya pembeni ya mji yanasogezewa huduma za afya kwa maana ya ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, tunamshukuru sana”.alisema Dk.Siwale
Hatahivyo alisema tayari serikali imetoa fedha kwaajili ya vituo vya afya katika kata ya Senga, achilia mbali kituo cha afya cha kata ya Sumbawanga ambacho kitajengwa na fedha za makusanyoi ya ndani za halmashauro hiyo.
Dk.Siwale alisema kuwa ongezeko hilo la vituo vya kutolea huduma ndilo linaongeza mahitaji ya watumishi wa Idara hiyo ikiwa ni pamoja na Madaktari, Wauguzi, Mafundi sanifu wa maabara, pamoja maeneo mengine mengi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya ,ujenzi wa hospitali ya wilaya ya halmashauri hiyo eneo la Isofu utakwenda sanjari na unjenzi wa barabara ya lami ya kilometa mbili kwenye barabara ya kuingia na kuzunguka eneo hilo la hospitali ili kurahisisha utoaji wa huduma pamoja kujenga unadhifu wa maeneo hayo.
Mtalitinya ambaye naye hakuishiwa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendele kutoa fedha za ujenzi hospitali hiyo ambayo ni muhimu kwa wakazi wa mji wa Sumbawanga kwakuwa itapunguza msongamano katika hospitali tegemezi kwa sasa ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa.
Mtalitinya alisema ili kuendelea kuboresha huduma katika hospitali hiyo ya Isofu, halmashauri imeingia mkataba na Shirika la Nyumba kwaajili ya ujenzi wa nyumba za kisasa kwenye eneo hilo, lakini pia maeneo ya huduma zingine kama vile viwanja vya michezo vya kisasa vitajengwa maeneo ya pembeni ya hospitali hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Sumbawanga mjini Aesh Hilaly alisema huduma za afya katika halmashauri hiyo zinaendelea kuboreshwa kulingana na jiografia ya maeneo husika ili kuzidi kuzisogeza karibu.
Aesh alisema katika mwaka huu wa fedha wanatarajia kupata fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati za kijiji cha Milanzi na kujenga zahanati na Kinamwanga ambazo zimeanza kujengwa zikiwa kwenye hatua za awali.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa