Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya ameelezea mpango wa halmashauri wa kuhakikisha kila kata inakuwa na soko la kisasa ili kusogeza huduma kwa wananchi wanaoishi katika kata hizo na kutanua makazi yam ji kwa ujumla.
Amesema kuwa mpango huo unasura inayofanana na masoko yalivyopangiliwa katika mkoa wa Dar es salaam ambapo kila mahali panakuwa na soko kulinagana na mji unavyokuwa huku akitilia mkazo kuanza na ujenzi wa soko la kisasa la mandela na masoko mengine yatafuata kwa awamu.
“Sura tunayoitazama ya kuboresha masoko ni kama ilivyokuwa namna ya kuboresha masoko ya Dar es salaam kwamba kuwa na program ya kujenga masoko katika maeneo mbalimbali kulingana na mji unavyokuwa sisi tumeandaa andiko ambao linalenga kujenga masoko katika maeneo mbalimbali kama sita kwa sasa na baadae tutamilia kata zote,” alifafanua.
Mtalitinya alitoa maelezo hayo wakati akijibu swali la Mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara mkoa ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Jaochim Wangabo juu ya uboreshaji wa masoko pamoja na barabara zinazotoka kwenye masoko mbalimbali yayopo kwenye manispaa hiyo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa