Idara ya Kilimo ya Manispaa ya Sumbawanga imepata mwaliko wa kutembelea Bonde la Ziwa Rukwa katika kijiji cha Kapenta kwaajili ya kwenda kutoa elimu ya upandaji wa mboga aina ya Broccol (Brokoli) ambayo inapendwa na familia moja yenye asili ya Kimarekani wanaoishi huko.
Mwaliko huo unafuatia ziara ya Mkurugenzi wa Kikundi cha Hodari Group Tedi Paulo Rabenold ambaye alifika kwenye Banda ka Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya la Manispaa ya Sumbawanga na kujionea vipando mbalimbali vilivyoandaliwa.
Banda ka Manispa ya Sumbawanga ambalo lipo upande Kaskazini Mashariki mwa uwanja huo wa Maonesho hayo karibu na kituo bubu cha treni, licha ya kuwa na bidhaa mbalimbali ambazo ziko ndani ya banda hilo lakini kwa nje kuna vipando vya mbogamboga na mazao mengine kama ngano, alizeti, vitunguu, Pilipili Hoho, nyanya na mahindi.
Ujio wa Tedi kwenye eneo hilo ulimshangaza kukutana na mboga jiyo aina ya Brokoli ambayo alisema kuwa ni mboga kipenzi kwa familia yake hususan mkewe ambaye hulazimika kusafiri hadi Jijini Dar es salaam kuitafuta katika Super market.
“Mimi nilikuwa sijui kuwa nyie Wataalamu wa Manispaa ya Sumbawanga kuwa mnaweza kuzalisha hii mboga, maana ni mboga nzuri, nashauri endelea kuwaambia watu uzuri mboga hii na faida yake katika lishe, hongereni sana”.alisema Tedi
Hatahivyo Tedi aliwaomba Wataalamu hao kutembelea nyumbani kwake ili waweze kutoa ujuzi huo katika kupanda na kuitunza mboga hiyo.
Mboga aina ya Brokoli kwa mujibu wa Wataalamu inathamini kuwa katika mwili wa binadamu kwa mtumiaji anaweza kujikinga dhidi maradhi ya moyo, kuzuia utapiamlp kwa watoto, ambapo unaweza kuipika kwa kuchanganya na nyama au kwenye mboga zingine na hata pekee yake.
Kwa taarifa zaidi tembelea Banda la Manispaa ya Sumbawanga ambapo utaonana na Wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa Jacob Mtalitinya.
Licha ya mambo mambo mengineyo kikundi cha Hodari Group cha wilayani Sumbawanga kinachoongozwa na Tedi kinajishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali ya matunda kama vile Nazi, Mapapai, Ndimu, Mananasi na machungwa katika Bonde la Ziwa Rukwa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa