Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imezidi kupanua wigo wa utoaji huduma kwa sekta ya afya kwenye halmashauri hiyo baada ya kufunguliwa kwa hospitali mpya ya wilaya ya halmashauri hiyo na zahanati moja zaidi.
Kufunguliwa kwa halmashauri hiyo kunafuatia taarifa ya Mkurugebzi wa halmashauri hiyo Jacob Mtalitinya ambaye amesema kuwa hospitali ya wilaya iliyopo eneo la Isofu inafunguliwa baada ya kukamilika kwa baadhi ya majengo ya kutolea huduma.
Mtalitinya alisema kuwa ameridhishwa na ukaguzi na maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo na ushauri na Wataalamu wa afya ambao taarifa yao inaonesha kuwa vifaa tiba vilivyopo vinaweza kuanza kutoa huduma kwa kiwango bora.
Mkurugenzi alisema hospitali hiyo ambayo imeanza kutoa huduma na alizitaja huduma zitakazoanza ni pamoja na wagonjwa wa nje, huduma ya Baba, Mama na mtoto, huduma ya Maabara na upimaji wa virusi vya Ukimwi.
Mtalitinya alisema kuanza kufanya kazi kwa hospitali hiyo kunasogeza huduma maeneo ya karibu zaidi kwa wananchi ambapo awali Manispaa hiyo ilikuwa ikitegemea kupata huduma katika ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na hospitali Teule ya Dk.Atman iliyopo mjini Sumbawanga.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa licha ya kufunguliwa kwa hospitali hiyo pia jitihada zimefanyika za kuzidi kuimarisha utoaji wa huduma katika ngazi ya vijiji na hivi sasa katika tarehe hiyo pia kutafunguliwa zahanati ya kijiji cha Nambogo ambayo iko kwenye kata ya Milanzi.
Katika zahanati hiyo nako huduma zitakazotolewa ni pamoja na wagonjwa wa nje, huduma ya Baba, mama na mtoto pamoja na maabara.
Licha ya huduma hizo ambazo zinafunguliwa, Manispaa hiyo hivi sasa inajenga vituo vya Afya viwili katika Kata za Mollo na Matanga,lakini pia zahanati ya kijiji cha Mponda na Pito, huku Mkurugenzi Mtalitinya akimshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa vituo hivyo vya afya na zahanati.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa