Halmashauri ya Manaispaa ya Sumbawanga imetoa mikopo yenye thamani ya Tsh Milioni 136,982,449 kwa vikundi vya kina mama, vijana na Watu wenye ulemavu katika kipindi cha Julai – Desemba 2022.
Akiyasema Hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mansipaa ya Sumbawanga Ndugu Jacob J Mtalitinya katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya Oktoba Desemba 2022 amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeendelea kutekeleza sera ya uwezashaji wananchi kiuchumi kwa lengo la kuwa kwamu wananchi na wimbi la umasikini na utegemezi kwa kuwapa na kuimarisha mitaji ya vukundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu .
Katika fedha hizo zilizotolewa kiasi cha Tshs Milioni 45,200,000 zilitolewa kwa kuwapa Umoja wa Waendesha Bajaj vyombo vya usafiri ikiwa ni bajaj ambazo imeshasajiliwa na kukatiwa bima na kiasi cha Tshs Milioni 91,782,449 zilitolewa kama fedha taslim kwa ajili ya kuimarisha mitaji na kuongeza wigo wa biashara za vikundi vya wajasiriamali vya wanawake .
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga amesema kuwa hadi kufikia mwezi Julai wana uhakika kuwa kiasi cha asilimia kumi kilichotengwa katika bajeti yam waka 2022/2023 kitakuwa kimetolewa kwa walengwa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa