Zaidi ya Shilingi Milioni 800 zimetumika kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu na ulipaji wa madeni mbalimbali ya Walimu katika Idara ya Elimu Msingi kwa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Fedha hizo ni pamoja na malipo ya Walimu kwaajili uhamisho na likizo ambayo walikuwa wakidai kwa muda mrefu.
Akizungumzia mafanikio ya Mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Afisa Elimu Msingi Robert Tarimo alisema jumla ya Sh.813,315,140 zimetolewa, kati ya hizo Shilingi Milioni 89.7 zimetumika kwaajili ya malipo ya uhamisho kwa Walimu na Sh.141.9 Milioni zimetumika kwa malipo ya madai ya likizo
Tarimo aliendelea kufafanua kuwa katika kuimarisha elimu ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu serikali imetoa Sh.160 Milioni kwenye fedha za Uviko-19 ambazo zimetumika kwaajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi kwenye Shule ya Msingi Kizwite na Malangali ambayo imepata fedha za LANES II kwa mgao wa kila shule Milioni 80 kwaajili ya kazi hiyo.
Kwa upande wa vyumba vya madarasa Afisa Elimu huyo wa Elimu Msingi alisema Manispaa hiyo ilipokea jumla ya Shilingi Milioni 100 ambazo zimetumika kukamilisha ujenzi wa madarasa kwenye shule tofauti katika halmashauri hiyo ikiwa ni ruzuku ya serikali.
Manispaa hiyo pia ilipokea Shilingi Milioni 101.6 kutoka Mfumo wa kunawa mikono COVID-19.
Katika kuimarisha miundombinu ya madarasa Tarimo alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imepokea na kujenga vyumba vinane vya madarasa katika Shule za Msingi Matanga, Kankwale,Mawenzusi na Utengule kwa kila shule kupata Shilingi Milioni 60 kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kila shule, isipokuwa Utengule pekee ambayo ilipokea kiasi cha Shilingi Milioni 40 kwaajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
Aidha Afisa Elimu Tarimo ameishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zimetatua baadhu ya changamoto katika sekta ya elimu Msingi katika Manispaa ya Sumbawanga.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa