By Kisika S.- Kitengo cha Mawasiliano SMC
Diwani wa Kata ya Katandala Edwine Amando Misasi amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Misasi amechaguliwa katika nafasi hiyo akiwa ni mgombea pekee kutoka CCM ilihali Diwani pekee kutoka CHADEMA ambaye anawakilisha kata ya Kizwite Andrew Cheka yeye hakugombea nafasi hiyo kuwakilisha upande wa pili.
Akitangazo matokeo ya uchaguzi huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Pendo Mangali aliutaja ushindi wa kura zote 23 za Madiwani walioshiriki uchaguzi huo kuwa zilimpa ushindi Misasi.
Akisherehesha ushindi wake Naibu Meya huyo alisema kuchaguliwa kwake kutakuwa na tija iwapo atapata ushirikiano kutoka kwa Madiwani wenzake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo lengo lake kubwa nikuiletea maendeleo.
Misasi anakuwa Naibu Meya wa Nne kwa kipindi cha 2020 hadi 2024 na atahudumu katika nafasi hiyo hadi mwakani kabla uchaguzi mkuu.
Wengine waliowahi kuongoza nafasi hiyo wakimsaidia Mstahiki Meya Justine Malisa katika nafasi ya Unaibu Meya ni Istusi Kapufi (Matanga), Juma Mnanka (Msua) na Frank Lupimo (Milanzi).
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa