• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Manispaa
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Masuala ya Lishe
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Uratibu na Mipango
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasimali watu
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati na majukumu yake
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi, Elimu & Afya
      • Mipango miji & Mazingira
    • Ratiba za Vikao
      • For Councilors
      • For Hon. Mayor
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
    • Huduma za Kisheria
    • Fedha
  • Kituo cha Habari
    • Albamu ya Picha
    • Video
    • Taarifa Kwa Umma
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Makala
    • Michezo & Burudani

Michango yamuweka matatani Mkuu wa shule ya Muhama

Ilibandikwa: February 4th, 2018

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameagiza mkuu wa shule ya sekondari Muhama Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa kuchukuliwa hatua kwa tuhuma za kuwatoza wanafunzi michango ya Sh5,000 kama gharama ya kuwapatiwa fomu za maelezo ya kujiunga na shule hiyo.

“Hili suala la kuchangia maendeleo halikuanza jana wala juzi lakini suala hili limeporwa na viongozi wa shule, nao wanafanya kama mitaji yao, wananchi tunawaambia wachangie kwa hiyari yao lakini waelekeze kwa Mkurugenzi na sio kiongozi yeyote wa shule. Nakuagiza mkurugenzi kuchukua hatua katika hili na ninataka nipate taarifa’,” alisema.

Na kusisitiza kuwa ili kuwaepusha wazazi na michango Halmashauri hazina budi kuhakikisha kuwa zinaongeza vyanzo vya mapato ili kusaidia miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea kwenye halmashauri hizo.

Mh. Wangabo ametoa agizo hilo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kata ya Malangali baada ya baadhi ya wananchi kufichua jambo hilo, walipopewa ruhusa ya kueleza kero zao na Mkuu huyo wa mkoa.

Mmoja wa wananchi hao, Sadock Kalinga amesema wazazi wamekuwa wakichangishwa kiasi hicho cha fedha ili wapatiwe fomu hizo.

“Tulilazimika kutoa fedha hizi na kupewa stakabadhi kwa kuwa tuliambiwa mwanachi ambaye hatotoa fedha hawezi kupewa fomu hizo na hivyo kukosa sifa ya kujiunga katika shule hii,” amesema Kalinga.

Baada ya kupokea malalamiko hayo na kuonyeshwa risiti iliyotolewa kama ushahidi, Wangabo amemhoji Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga, Hamidu Njovu kuhusu uhalali wa mchango huo ambapo naye alikana kufahamu jambo hilo.

Matangazo

  • TANGAZO LA CHANJO KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO April 26, 2023
  • RATIBA YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2023 March 11, 2023
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2023 March 11, 2023
  • TANGAZO LA ZABUNI YA KAZI ZA UBORESHAJI WA BARABARA KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA March 01, 2023
  • Angalia zote

Habari za Karibuni

  • SHIRIKIANENI NA SERIKALI KULETA MAENDELEO RUKWA-RC MAKONGORO

    March 16, 2025
  • MD PENDO MANGALI-MSIWE MADALALI WA VIWANJA, CHAPENI KAZI

    November 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA SUMBAWANGA

    October 01, 2024
  • EDWINE MISASI NAIBU MEYA MPYA MANISPAA YA SUMBAWANGA

    August 27, 2024
  • Angalia zote

Video

MANISPAA YA SUMBAWANGA KUTAFUTA MZABUNI WA KUZOA TAKA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • History
  • Councilors
  • Photo Gallery

Viunganishi vinavyofanana

  • Public Servant portal
  • Download your Salaryslip here
  • Looking for a job in Public Sector?
  • Get everything from the government
  • Rukwa
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Sumbawanga Municipal Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga

    Simu ya Mezani: +255252802163

    Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255

    Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Uhuru binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa