Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inakusudia kuanzisha mfuko Maalumu wa elimu kwaajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye shule za Msingi na sekondari.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt.Halfan Haule wakati mkutano wa Wadau wa Elimu wa halmashauri hiyo uliofanyika Februari 20, kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Dkt,Haule alifikia maamuzi hayo ikiwa ni kukiubaliana na michango ya mawazo ya mmoja ya wajumbe Emmanuel Mwakamwelo ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mazwi ambaye alishauri kuwa ni vyema ukaanzishwa mfuko huo.
“Nimekubaliana na mawazo hayo na nimwagize Mkurugenzi kufanya haraka ili mfuko huu uweze kuanzishwa, kwani natambua umuhimu wake kwasababu shule zetu zinakabiliowa na changamoto za uchakavu wa madarasa, madawati, vyoo na mambo mengine mengi.”alisema.
Kwenye mkutano huo Mkuu huyo wa wilaya aliwaasa Walimu kushirikiana kwa kufundisha wanafunzi ili waweze kupata matokea chanya kwenye shule zao.
Aidha aliwataka Walimu kuzingatia maadili ya kazi zao na kuepukana na vishwawishi wanavyokutana navyo sehemu zao za kazi.
Hatahivyo kwenye mkutano huo baadhi ya shule za Msingi na Sekondari zilipatiwa zawadi ya fedha na vyeti ikiwa ni ishara ya kutambua jitihada zao katika kufaulisha wanafunzi.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa