Jamii wilayani Sumbawanga imeombwa kujitolea kusaidia kutatua changamoto za miundombinu kwenye Shule za Msingi na Sekondari ambazo wanafunzi wake wamekuwa wakishindwa kusoma vizuri kwa kukosa baadhi ya vifaa.
Ushauri huo umetolewa na Katibu Tawala wa wilaya ya Sumbawanga Shaban Sebabili wakati akikabidhi msaada wa madawati 20 yalitolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kanda ya Mbeya kwa Shule ya Msingi Momoka mjini Sumbawanga.
Sebabili alisema kuwa tatizo la madawati bado ni kubwa katika shule za Mnispaa ya Sumbawanga huku akibainisha kuwa upungufu uliopo ni zaidi ya madawati Elfu 6.6, hivyo kutoa wito kwa wadau kusaidia kutatua changamoto hiyo.
Aida aliishukuru BOT kwa kutoa msaada huo huku akiwaomba wadau nao kuguswa na tatizo la wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati.
Diwani wa kata ya Sumbawanga Cornel Kufumu licha kuonesha furaha yake kwa kupata msaada huo lakini pia aliishukuru serikali na Wadau hao na kuongeza kuwa msaada unahitajika zaidi kwenye shule hiyo ya Momoka ambayo vyumba vyake vingi vya madarasa vimechakaa kutokana kujengwa siku nyingi.
Kwa upande wake Afisa Msingi wa Manispaa ya Elimu Mussa Musoma alisema wameweka mkakati wa kupunguza changamoto hiyo kwa kufanya vikao na wazazi wa shule mbalimbali ili waweze kujitolea kutengeneza madawati kupitia program ya UWAWA, lakini pia wamekuwa wakiwasiliana TSF ili waweze kuwasaidia kupata mbao za kutengeneza madawati kwenye shule hizo ambazo nyingi hazina madawati ya kutosha.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa