Baraza la Madiwani Manispaa ya Sumbawanga imepitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti kiasi cha Tsh bilioni 44,008,689,000 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri.
Akiwasilisha bajeti hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Ndg. Jacob J. Mtalitinya amesema kuwa kiais cha Tsh Bilioni 10,356,239,000 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleokwa Sekta ya Elimu na Afya.
Kati ya Tsh Bilioni 44 ,008,689,000 Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inatarajiwa kukusanya kiasi cha Tsh Bilioni 3,408,124,600 ikiwa ni mapato ya ndani saw ana ongezeko la asilimia 36.5 ukilinganisha na kiasi kitachokusanywa katika mwaka wa fedha 2022/2023 kama mapato ya ndani.
Katika fedha za mapato ya ndani Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imetenga kiasi cha Ths Milioni 800,332,000 sawa na asilimia 40 ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa