Anaandika Sammy Kisika.
Wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Rukwa wameoneshwa kuhuzunishwa kwao na namna Wizara ya Ujenzi inavyochelewesha kuanza kwa shughuli ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa uwanja wa ndege wa Sumbawanga ambao kwa muda mrefu umekuwa ukitajwa kuwa utajengwa.
Mwenyekiti wa kikao cha Road Board ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti amesema hali inaonesha kuwa wananchi mkoani Rukwa wamechoshwa na ahadi za mara kwa mara kuhusu ujenzi wa uwanja huo ambao tayari wananchi waliokuwa pembezoni mwa uwanja wamekwishalipwa fidia takribani miaka mitatu iliyopita.
Mkirikiti amesema pamoja na kuwalipa fidia wananchi hao lakini pia Mkandarasi wa kujenga uwanja huo alishapatikana ambaye ni M/S Sino-Shine Overseas Construction & Investment East Africa Ltd kwa thamani ya Shilingi Bilioni 55.
Amesema kucheleweshwa kwa ujenzi wa uwanja huo kumekuwa kukileta adha kubwa kwa wasafiri na huduma za ndege kwa mkoa wa Rukwa ambapo wananchi wanalazimika kwenda kupanda ndege mikoa jirani ya Songwe na Katavi.
“Ufike muda sasa tuachane na maneno, wananchi waambiwe ukweli kuwa ni lini kazi hii inaanza lakini siku zote wamekuwa wakipewa ahadi ya siku za karibuni kazi itaanza na hakuna kinachofanyika”.aliema Mkirikiti akiungwa mkono na wajumbe wa kikao hicho.
Uwanja wa ndege wa Sumbawanga umekuwa ni jambo ambalo limekuwa likizungumziwa kwenye vikao mbalimbali vya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Sumbawanga na hata vikao vya Kamati ya Ushauri ya mkoa (RCC) ambapo siku zote
Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Rukwa Eng. Jofrey August amesema ujenzi wa uwanja huo kwa kiwango cha lami utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege na viungio vyake, jengo la abiria, barabara za kuingilia uwanjani, sehemu ya kuegesha ndege na magari, mnara wa kuongozea ndege na hali ya hewa na usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege.
August amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 serikali Shilingi Bilioni 2.8 kwaajili ya kuanza kazi hiyo ambapo katika ya hizo Milioni 110 ni fedha za ndani na Bilioni 2.7 ni fedha kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya ( European Investment Bank).
Tayari kiasi cha Shilingi Bilioni 3.7 zilikwishalipwa kwa wananchi ambao walitakiwa kuondoka kupisha upanuzi wa uwanja huo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa