Msimu wa kilimo 2016/2017 Halmashauri ya Mnispaa ya Sumbawanga ililenga kulima jumla ya hekta 58,188 za mazao mbalimbali kati ya hizo hekta 34,851 ni za mazao ya jamii ya nafaka, hekta 1,940 za mazao ya jamii ya mizizi, hekta 14,808 ni mazao ya jamii ya mikunde na hekta 5,720 za mazao ya mafuta.
Lengo la mavuno lilikuwa ni tani 146,203 kwa mazao yote kwa ujumla ambapo kati ya hizo tani 102,491 ni za mazao ya nafaka, 12,767 ni za mazao jamii ya mizizi, tani 17,757 ni za mazao jamii ya mikunde na tani 6,828 ni ya mazao ya mafuta. Katika kutekeleza malengo hayo, jumla ya hekta 58,025.3 zililimwa ambapo kati ya hizo hekta 34,759 za mazao ya nafaka, hekta 1,946 za mazao ya mizizi, hekta 5,728 za mazao ya mafuta na hekta 14,808 za mazao ya mikunde.
Mavuno yalikuwa tani 144,867.95 ambapo kati ya hizo tani 102,299.4 zilikuwa za mazao ya nafaka, tani 12,807 za mazao ya mizizi, tani 6,837.8 za mazao ya mafuta na tani 17,758.2 za mazao ya mikunde.
Idadi ya watu katika Manispaa ya Sumbawanga ni 209,793 kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, ambapo kwa mwaka huu 2017 inakadiriwa kuwa na ongezeko la idadi ya watu wapatao 250,165 hivyo, mahitaji ya chakula kwa mazao ya nafaka ni tani 75,049.5 na mikunde ni tani 25,016.5 kwa hiyo kipo chakula cha kutosha na ziada ya tani 27,249.9 za nafaka na tani 7,257.8 za mikunde.
Katika msimu wa mwaka 2017/2018 Manispaaa inalenga kulima jumla ya hekta 58,029 za mazao mbalimbali kati ya hizo hekta 26,186.3 ni za mazao ya nafaka, hekta 2,369.1 ni za mazao ya mizizi, hekta 4,862.4 ni za mazao ya mafuta, na hekta 22,380 ni za mazao ya mikunde.
Malengo ya mavuno ni jumla ya tani 149,542 kati ya hizo mazao ya nafaka ni tani 88,268.26 mazao ya mizizi ni tani 15,767.9 mazao ya mafuta ni tani 3,698.7 na mazao ya mikunde ni tani 26,684.7.
Kwa msimu wa mwaka 2017/2018 mahitaji ya pembejeo ni kama ifuatavyo, mbolea ya kupandia (DAP) tani 6,009 mbolea ya kukuzia (UREA na CAN), tani 6,009 na mahitaji ya mbegu zao la mahindi ni tani 581 na mazao mengine ni tani 2,694. Shughuli za kilimo kwa kiasi cha asilimia zaidi ya 85 kunategemea zana zinazokokotwa na ng’ombe (maksai) kilimo kwa kutumia zana za kisasa (matrekta) ni kwa kiwango, kwani mpaka sasa yapo matrekta 32 katika Halmashauri nzima.
Halmashauri inaendelea kuhamasisha wakulima wajiunge katika vikundi (AMCOS) ili waweze kuchangia mitaji na kuweza kukopeshwa matrekta ambayo yatachangia kuongeza uzalishaji na kupunguza harupu kwa wakulima.
Ili kuweza kufikia malengo hayo hapo juu, Halmashauri imejipanga kufanya mambo yafuatayo:
Kuna changamoto ya soko la zao la mahindi ambapo kwa sasa ni kati ya shilingi 30,000 hadi 42,000 kwa gunia la kilo mia moja na bei ya maharage ni kati ya shilingi 120,000 hadi 180,000 kwa gunia la kilo mia moja na bei ya mpunga ni kati ya shilingi 75,000 hadi 90,000 kwa gunia la kilo 75.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa