Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya ameondoa sintofahamu iliyokuwa imesambaa katika manispaa hiyo juu ya maagizo na maelekezo mablimbali aliyoyatoa katika kuboresha huduma kwa kukusanya mapato na kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kujiboreshea maisha katika manispaa hiyo.Mtalitinya alisema kuwa sula la vibali vya ujenzi na leseni za makazi imetafsirika tofauti lakini azma ni kuipima Manispaa kwa asilimia 100 na kuwa huo ni mwendo wa kufanya upimaji.
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeibuka mshindi wa kitaifa wa mbio za za Mwenge wa Uhuru uliowashwa mwezi April katika viwanja vya magogo Mkoani Geita na na kuzimwa mwezi oktoba siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Julius Nyerere katika Kiwanja Mkwakwani Mkoani Tanga na kukimbizwa katika Halmashauri 195 nchini.
Mradi wa upimaji viwanja Nambogo na Katumba Azimio umetekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), hii itasaidia upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa na kuwekewa miundombinu ya msingi na kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi waishio katika kata za pembezoni za Pito, Molo, Milanzi, Lwiche nk.Jumla ya viwanja 2161 vimepimwa katika eneo hilo la Nambogo na Katumba Azimio kwa matumizi mbalimbali ikiwemo makazi, makazi na biashara, shule, huduma za afya, maofisi, kituo cha biashara (Shopping Mall), vituo vya mafuta, viwanja vya michezo na maeneo ya kupumzikia.viwango vya matumizi ya viwanja.Na Aina ya matumizi Gharama kwa kila mita ya mraba1 Makazi pekee (ujazo wa juu, kati na chini 2,700/=2 Makazi na biashara 3,000/=3 Biashara 5,000/=4 Huduma za jamii 3,500/=5 Ibada/ kuabudu 3,500/=6 Hoteli, vituo vya mafuta na maduka ya kuiwekezaji 5,000/=Wahi kuchukua fomu katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanaga na kupitia tovuti ya www.sumbawangamc.go.tz
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: 0784519681
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa