Mafunzo mbalimbali yanayoendelea kutolewa na Manispaa ya Sumbawanga kuongeza uelewa wa sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji
Kutoa elimu ya biashara kwa vijana
Kwa kushirikiana na Taasisi zingine za umma kama SIDO, VETA na Vyuo vya kilimo; Manispaa itatoa mafunzo juu ya;-
a) Kuboresha shughuli za uzalishaji wa mazao ya kilimmo na mifugo
b) Usindikaji wa mazao ya mifugo na kilimo
c) Kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo na mifugo,
d) Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali mfano sabuni, madawa ya chooni, ufumaji na ushonaji wa nguo, utengenezaji wa viatu nk.
e) Utengenezaji wa zana za kilimo
f) Utengenezaji wa vifaa vya ujenzi kama vile tofali, chokaa, malumalu, vioo nk.
g) Kuweka kumbukumbu za biashara,
h) Elimu ya uongozi kwa vikundi vilivyoundwa
Mwaka 2017/18 Manispaa imetenga Tshs 1,400,000/- kwa ajili ya kutoa mafunzo juu ya usindikaji mazao kwa Wajasiliamali. Mafunzo yatatolewa na SIDO kwa Kushirikiana na Manispaa.
ii. Kuunganisha vijana katika vikundi
Ili kuwa na usimamizi mzuri na nguvu yenye msukumo katika masuala ya kibiashara za viwanda Manispaa itawaunganisha Vijana katika vikundi vya ushirika ambapo wataweza;-
a. Kukuza mitaji ya biashara kupitia mikopo itakayopatikana kwa urahisi kwenye Taasisi za fedha, viingilio vya wanachama, ada, michango na hisa za wanachama.
b. Uundwaji wa ushirika mkubwa utakaosimamia na kulea vikundi vidogovidogo vya ushirika ambacho kitakuwa ni chombo kikuu na sauti ya wafanyabiashara kwa kusimamia utoaji wa mikopo na uendeshaji wa vikundi vya ushirika ndani ya Manispaa
iii. Kuunganisha vijana na taasisi za fedha
Vijana na wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa mitaji ya kutosha kuendesha biashara zao. Kwa kuwa uwezo wa Manispaa ni mdogo hasa mapato yake ya ndani kuwezesha wafanyabiashara wote hivyo Manispaa itawaunganisha wafanyabiashara kupitia umoja wao uliosajiliwa (Ushirika) na Taasisi za fedha ambazo zinatoa mikopo kwa masharti nafuu. Ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya uchaguzi na maamuzi ya Taasisi wanazotaka kuchukua mikopo Manispaa itakuwa na jukumu la kutafsiri Sera na Miongozo kwa wafanyabiashara wadogodogo.
Halmashauri inalengo kuu la kuanzisha Benki ya Wananchi wa Manispaa ambayo umiliki wake utajumuisha umoja wa wafanyabiashara hasa wadogowadogo (Wakulima, Wafugaji, Mamalishe, Waendesha Bodaboda na Bajaji, Machinga, Vikundi vya vijana na wanawake n.k). mfano wa benki za aina hii ni “Mufindi Community Bank”, “Dar Es Salaam Community Bank” na “Mwanga Community Bank”.
iv. Kutoa taarifa za masoko
Ili wafanyabiashara Vijana waweze kufanya biashara kulingana na mahitaji ya soko Manispaa itakuwa na jukumu la kutafuta taarifa za biashara na masoko na kuwapatia wafanyabiashara. Taarifa za kibiashara zitakazotafutwa na Manispaa kwa ajili ya wafanyabiashara ni kama ifuatavyo:-
a. Bei ya bidhaa
b. Mahitaji ya bidhaa katika viwanda vilivyopo,
c. Ubora wa mali ghafi zinazohitajika viwandani
d. Usafirishaji
e. Walaji
v. Kudhibiti na kukagua hesabu za vikundi
Ili kujiridhisha na usimamizi, matumizi ya rasilimali fedha na kuhakikisha uendelevu wa vikundi unakuwepo Manispaa itahakikisha inasimamia zoezi la kufanya ukaguzi na kutekeleza ushauri wa wakaguzi. Ukaguzi utafanywa na wakaguzi wa ndani na wakaguzi walioidhinishwa na Serikali (COASCO).
vi. Kufanya tafiti za kibiashara na masoko
Ili kuendana na mahitaji ya sasa kulingana na sayansi na teknolojia Manispaa itakuwa na jukumu la kufanya tafiti za kibiashara na masoko ili kujua fursa mpya za biashara na masoko. Kwa mfano;-
a. Hitaji la kuanzisha biashara mpya tofauti katika eneo letu kwa mfano kilimo cha maua, vanilla, kilimo cha mbogamboga kulingana na mahitaji ya nchi jirani.
b. Kufanya tafiti za uwezo na uhitaji wa kuwa na eneo moja au kikundi kimoja kinachozalisha bidhaa ya aina moja (One District One Product)
vii. Kukuza jitihada za ubunifu
Ili kuhakikisha maendeleo ya Manispaa yanakuwa endelevu, uwekezaji katika sayansi na technolojia nafuu inayobuniwa na kusanifiwa Wilayani ni muhimu sana. Hali ilivyo sasa ni kwamba wapo Vijana na Wanawake wanaofanya shughuli mbali mbali kwa kutumia vipaji vyao lakini hawajatambuliwa na kuunganishwa na mitaji na masoko ili kuboresha shughuli wanazofanya na kuendeleza ubunifu wao. Ubunifu uliyopo sasa ni utengenezaji wa zana za kilimo, viatu, ushonaji mavazi, na utengenezaji wa mapambo ya nyumbani kwa kutumia udongo mfinyanzi. Kwa Mwaka 2017/18 Manispaa imetenga Tshs 10,000,000/- kwa ajili ya kuinua vipaji na jitihada za ubunifu.
Idadi ya Waliopewa Leseni za Biashara kuanzia 2014/2015-2016/2017
No
|
Aina ya Biashara |
Idadi ya Waliopewa Leseni za Biashara |
||
2014/2015 |
2015/2016 |
2016/2017 |
||
1
|
Sub whole shops
|
5 |
9 |
12 |
2
|
Retail shops
|
579 |
605 |
718 |
3
|
Milling machines
|
110 |
145 |
168 |
4
|
Textile and garments retail
|
130 |
192 |
256 |
5
|
Guest houses
|
70 |
78 |
93 |
6
|
Selling medicines retail
|
40 |
52 |
85 |
7
|
Dispensaries (private)
|
4 |
5 |
6 |
8
|
Butchery shops
|
28 |
32 |
69 |
9
|
Restaurants
|
8 |
14 |
27 |
10
|
Selling of bicycle spare parts retail
|
6 |
9 |
12 |
11
|
Second hand clothes retail
|
56 |
73 |
88 |
12
|
Hardware and building materials retail
|
18 |
28 |
41 |
13
|
Kiosk/groceries
|
310 |
403 |
572 |
14
|
Crop buying
|
39 |
51 |
75 |
15
|
Soft drink agents
|
11 |
18 |
23 |
16
|
Photo studios
|
6 |
6 |
9 |
17
|
Welding works
|
20 |
33 |
62 |
18
|
Garages
|
5 |
8 |
12 |
19
|
Selling of fish
|
9 |
13 |
21 |
20
|
Petrol and filling stations
|
5 |
7 |
11 |
21
|
Timber and furniture retail
|
22 |
31 |
44 |
22
|
Agricultural inputs
|
41 |
41 |
49 |
23
|
Bookstore and stationery
|
20 |
33 |
39 |
24
|
Hides buying
|
2 |
2 |
4 |
25
|
Livestock trading
|
2 |
3 |
5 |
26
|
Selling spare parts for motor vehicles
|
5 |
9 |
11 |
27
|
Medium scale industries
|
2 |
2 |
3 |
28
|
Itinerant trade
|
11 |
18 |
30 |
29
|
Hair saloon/barber shop
|
28 |
41 |
72 |
30
|
Selling spare parts for motor cycles
|
8 |
10 |
13 |
31
|
Building contractors
|
12 |
18 |
23 |
32
|
Household items
|
18 |
18 |
23 |
33
|
Tailoring shops
|
15 |
18 |
28 |
34
|
To show video pictures
|
3 |
9 |
11 |
35
|
Attended telephone offices
|
3 |
5 |
8 |
36
|
Lubricants
|
5 |
8 |
10 |
37
|
Carpentry
|
7 |
11 |
21 |
38
|
Tendering business
|
8 |
11 |
12 |
39
|
Charcoal
|
1 |
3 |
7 |
40
|
Auctioneer
|
2 |
3 |
3 |
42
|
Pool
|
- |
1 |
1 |
43
|
Voda shop
|
- |
1 |
1 |
44
|
Whole sale
|
5 |
6 |
7 |
45
|
Secretarial services
|
3 |
4 |
4 |
46
|
Broker
|
- |
1 |
1 |
47
|
Eye clinic
|
2 |
2 |
3 |
48
|
Entertainment Hall
|
3 |
3 |
3 |
49
|
Printing Press
|
2 |
2 |
2 |
50
|
Used spare parts
|
5 |
6 |
6 |
51
|
Electrical Equipment
|
6 |
8 |
10 |
52
|
Insurance Agent
|
2 |
2 |
3 |
53
|
Office Equipment
|
8 |
11 |
13 |
54
|
Agro vet
|
2 |
5 |
6 |
55
|
Internet services
|
1 |
2 |
2 |
56
|
Scrapper
|
3 |
6 |
7 |
57
|
M- Pesa shop
|
8 |
14 |
32 |
|
TOTAL
|
42 |
2,149 |
2,877 |
Source: Municipal Department of Industries and trade
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa