VIWANDA VILIVYOPO
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina jumla ya viwanda 493 vikihusisha viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kama inavyojionyesha hapo chini.
Na.
|
Aina ya Kiwanda
|
Uzalishaji
|
Idadi
|
1
|
Viwanda Vikubwa
|
Kiwanda cha Nyama, Unga na Maji
|
3
|
2
|
Viwanda vya Kati
|
Uzalishaji wa Unga
|
4
|
3.
|
Viwanda vidogo
|
Kukamua mafuta, ufundi na nafaka
|
486
|
|
JUMLA
|
493
|
Kiwanda cha Dew Drop
Energy Milling
SAAFI kiwanda cha Nyama, Sumbawanga
Manispaa imeandaa maeneo yafuatayo kwa ajili ya uendelezaji wa viwanda:-
Halmashauri imepima viwanja 153 vyenye ukubwa wa hekta 138.36 mita za mraba 560,000 katika kijiji cha Kanondo (Kanondo Industry Area) kwa ajili ya uwekezaji katika Sekta ya Viwanda. Jumla ya TZS 524M zimetumika kutwaa eneo la mradi, kugharamia upimaji na kuandaa michoro ya viwanja. Viwanja hivyo vipo hatua ya uuzaji kwa Wawekezaji mbali mbali. Pia, Manispaa inatarajia kupima viwanja 600 kwa ajili ya Viwanda na ujenzi wa Bandari kavu katika eneo la Makazi Mapya na Kijiji cha Mtimbwa. Juhudi za kukusanya pesa za kutwaa maeneo na upimaji zinaendelea.
Manispaa inatarajia kupima viwanja 200 kwa ajili ya viwanda na ujenzi wa bandari kavu katika eneo la makazi mapya katika kijiji cha Mtimbwa.
Uboreshaji wa Makazi
Uwepo wa Makazi Bora ni kichocheo muhimu cha kuvutia uwekezaji wa viwanda. Makazi Bora ni pamoja na uwepo wa nyumba za kuishi na hoteli za kufikia wageni.
Halamshauri inaboresha mji wa kuwa na mipango ya uboreshaji ifuatayo:-
MPANGO WA UZINDUZI WA KAMPENI YA UJENZI WA VIWANDA KATIKA HALMASHAURI.
Katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda Halmashauri imeweka utaratibu wa kuweza kufanya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa viwanda katika Manispaa ya Sumbawanga na kuweza kutoa elimu ya umuhimu wa kuweza kujenga viwanda ndani ya Manispaa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa