SUMBAWANGA MANISPAA NA FURSA ZA UCHUMI
STENDI YA KATUMBA YA AZIMIO
Mji wa Sumbawanga ni makao makuu ya Mkoa wa Rukwa
ambapo miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyoufanya mji wa Sumbawanga kuwa mji wa kuvutia na kupendeza ni manthari yake. Manthari inayojumuisha uwepo wa Stendi kubwa na ya Kisasa ya mabasi.
Stendi inayopatikana eneo Katumba Azimio lililopo Km 10 kutoka katikati ya mji wa Sumbawanga katika barabara ya Sumbawanga -Mbeya.Stendi Kuu ya Mabasi ya Katumba Azimo ina uwezo wa kuegesha mabasi 150 -200 kwa wakati mmoja.
Stendi hiyo ya kisasa ina jumuisha jengo la abiria lenye uwezo wa kupokea na kuhudumia abiria 1,200 kwa siku. Jengo hilo lina vyumba vya kukatia tiketi 23, eneo lililotengwa kwa matumizi ya Benki 01, eneo la mgahawa wa kisasa 01, vyumba vizuri vya kulala wageni 16, eneo la mazoezi 01, eneo la burudani (Club) 01, na Vyumba vya biashara mbalimbali 110.
Stendi hiyo ilianza kujengwa mwaka 2019 mwezi April kwa gharama ya Tsh 8,037,000,000/= (Bilioni Nane na Milioni Thelathini na Saba) ikiwa ambazo ni fedha za Mradi wa Uimarishaji Miji(ULGSP)kiasi cha Tsh5,500,000,000/= ( Bilioni Tano na Milioni Miatano ) fedha za Serikali Kuu Tsh2,500,000,000/= (Bilioni mbili na milioni miatano) na Fedha za Mapato ya ndani kiasi cha Tsh37,000,000/= (Milioni Thelathini na Saba) Stendi ilianza kutumika mnamo May mwaka 2021.
Stendi ya Katumba Azimio imekuwa miongoni wa vyanzo muhimu vya mapato vya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Pamoja na kuwa miundo mbinu ya stendi hii haitumiki kwa asilimia mia moja Halmashauri ya Mansipaa ya Sumbawanga imekuwa ikusanya kiasi kinachokadiriwa kufikia milioni mia tatu kwa mwaka.
Stendi ya Katumba Azimio imewezesha kukuwa kwa sekta ya usafirishaji ndani ya eneo la Manispaa ya Sumbawanga, na kuwezesha idadi kubwa ya vijana kujiajiri katika sekta ya usafirishaji kwa kutumia pikipiki maarufu kama boda boda, pikipipi za migu mitatu maarufu kama bajaj, daladala na tax ambazo zimekuwa zikchukua abiria kutoka eneo la stendi kwenda maeneo mbalimbali yam ji wa Sumbawanga.
Uwepo wa Stendi ya Katumba Azimio imekuwa kivutio kwa wawekezaji wa maneo ya nyumba za kulala wageni na maeneo mbalimbali ya huduma na biashara kuzunguka eneo la stendi.
Stendi ya Katumba Azimio inazo fursa za biashara kama vile huduma za kibenki, mgahawa, eneo la mazoezi, vyumba vya biashara na viwanja vya makazi, makazi biashara na biashara vinavyolizunguka eneo la stendi.
Halmashauri ya Mansipaa ya Sumbawanga inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka maeneo yote ya Tanzania nan je ya Tanzania kuwekeza na kufanya biashara katika eneo hilo la stendi.
“WEKEZA NASI, KUZA UCHUMI”
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa