Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanari Mstaafu Ngemela Lubinga ametoa wazazi kote nchini kushirikiana na wadau wengine katika kutatua changamoto ndogo ndogo zinazozikumbuka shule za Msingi na Sekondari badala ya kutegemea serikali ifanye kila kitu.
Wito wa Kanari Lubinga umetolewa baada ya kufanya ziara kwenye baadhi ya shule za Msingi mkoani Rukwa ambako alikuwa akiambiwa juu ya changamoto za vyoo vya wanafunzi na walimu, madawati na vitu vingine.
Katibu huyo wa siasa na Uhusiano wa Kimataifa alisema kuwa uzoefu unaonesha kuwa iwapo wananchi wakishirikishwa kwenye utatuzi wa changomoto hizo kunaweza kumalizwa matatizo hayo badala ya kukaa kusubiri serikali.
“Mimi niwahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Mlele ambako niliamua kutengeneza madawati ya mfano na kuyapeleka kwa wananchi ambao niliwaomba watoe mchango wao kwa kutengezneza dawati moja kwa kila mzazi na tukafanikiwa kuondoa changamoto ya madawati kwenye wilaya hiyo na tukawana ziada.”alisema Kanari Lubinga.
Alisema kuwachangisha wananchi sio mbaya lakini inapendeza iwapo watachangia vitu vinavyohitajika shuleni kuliko kutoa fedha ambazo baadhi ya watendaji wasiowaaminifu hawazifikishi sehemu husika, hivyo kuwavunja moyo wananchi kuendelea kuchangia.
Aidha amewataka wazazi kote nchini kuwahimiza watoto wao kwenda shule na wahakikishe wanasoma na kuwafundisha uzalendo ili waweze kukua pia kwenye maadili mazuri , badala ya kazi hiyo kuiiacha mikononi mwa Walimu pekee.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa