Wakazi wa mkoa wa Rukwa wameshauriwa kuendelea kuzitunza maliasili zilizopo ili mkoa huo uweze kupiga hatua kwa kuingiza kipato kinachotokana na sekta ya utalii kwa vivutio vinavyopatikana mkoani humo viweze kuleta tija kiuchumi.
Kauli ya Mkuu wa mmoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati wa uzinduzi wa ulinzi wa Maliasili za mkoa wa Rukwa, ulikwenda sanjari na uzinduzi wa filamu ya Royal Tour katika mkoa huo uliofanyika hii leo katika ukumbi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo.
“Tunaweza kuutangaza utalii na vivutio vyote vilivyopo mkoani Rukwa iwapo sote tutakuwa na kauli moja yenye mshikamano kwa kuyasimamia yale tunayopanga.
Mkirikiti alisema kuwa sekta hiyo ya utalii inmaweza kufanikiwa iwapo watumishi wa serikali na watu wote wa sekta binafsi watajitoa na kuona fursa zilizopo.
Hatahivyo alisema ipo haja ya wafanyabiashara mkoani Rukwa nan je ya mkoa wa kuwekeza katika mkoa kuwekeza kwa kuanza kujenga hoteli zenye kukidhi vigezo vya utalii ili hata pale wageni wanapokuja kuitembelea Rukwa wajisikie fahariya kufika.
Pamoja na yote alizitaka halmashauri zote mkoani Rukwa kutenga maeneo ya ujenzi wa vitega uchumi na kugawa kwa watu mbalimbali wenye kuonesha nia ya kuwekeza katika miradiu mbalimbali.
“Tatizo hapo ni kuwa maeneo yote mazuri ya kujenga hoteli utasikia limecxhukuliwa na baadhi ya watumishi wa halmashauri lakini hawayaendelezi, yatoeni kwa Wawekezaji badala ya kuyakumbatia na hamfanyi chochote” alisema Mkirikiti
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa