Serikali mkoani Rukwa imewatoa hofu wageni wote wanaosita kutembelea mkoa huu, wasiwe na wasiwasi wowote kwani hivi sasa ile sifa iliyokuwanayo ya uchawi haipo tena.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven alipozindua huduma ya madaktari bingwa chini ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), walioletwa mkoani Rukwa kutoa huduma mbalimbali kwa
wagonjwa kuanzia Julai 3 hadi 8, mwaka huu.
“Watu wengi bado wanaogopa kuja Rukwa kwa sababu wanazozijua wenyewe,nawaalika waje bila hofu kwa kuwa ile kitu (imani za kishirikina –uchawi) haupo na hivi sasa imebaki ni nadharia pekee, ambazo watu wanazizungumza pasipo ukweli wowote huku akiongeza kuwa sasa miundombinu ya barabara ni kwa kiwango cha lami,”alisisitiza.
Aliongeza kuwa hata uwanja wa ndege uliopo mjini Sumbawanga,unatarajiwa kukarabatiwa muda si mrefu na kuongeza kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa ndege kutakuwa na wigo mpana wa safari za kufika Sumbawanga kwani watu watakuwa na hiari ya kuchagua aina ya usafri wa kutumia aidha kwa gari au ndege.
Mh. Zelote aliongeza.."Njoo Sumbawanga, njooni Rukwa mamb ni shwari na hakuna wasiwasi wowote", huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuwapo katika eneo la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa
Madaktari bingwa saba wametoa huduma za magonjwa ya wanawake na mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo, mfumo wa pua , koo masikio na magonjwa ya moyo na ya ndani.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa