Uongozi wa Shule ya Wasiona ya Malangali Manispaa ya Sumbawanga umeiomba serikali kuongeza bajeti ya shule hiyo ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja bajeti ndogo ya chakula kwa wanafunzi.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Orthor Mkaranga alimweleza Mkurugenzi wa Mnispaa hiyo kuwa bajeti inayotolewa haitoshelezi kutokana kupanda kwa gharama vyakula lakini pia wanalazimika kuchukua kiasi cha fedha kwaajili ya kuwalipa Wapishi wanne wa shule hiyo.
Mkaranga alisema shule hiyo pia inachangamoto ya kukosa wa usalama wa kutosha kwa wanafunzi na mali za shule hiyo kutokana uzio uliopo kutokamilika, licha kuishukuru serikali kujenga uzio huo ambao kilikuwa ni kilio chao cha muda mrefu.
Shule hiyo ambayo ina wanafunzi wasiona na walemavu wa ngozi pia inakabiliwa na uhaba wa Walimu, sanjari na kukosekana kwa choo kwenye bweni la wanafunzi na kukosekana kwa ulinzi nyakati za mchana, huku akilisemea pia tatizo la uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo, jambo lililoungwa mkono na Diwani wa Kata ya Malangali Mary Kipalasha.
Akikabidhi mashine maalumu za kusomea 24 za Orbit 20 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 46 kwa shule hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Catherine Mashalla alisema serikali imekuwa ikijitahidi kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari hivyo hata changamoto zilizopo kwenye shule hiyo zitaendelea kutatuliwa kwa awamu.
Mkurugenzi huyo wa Manispaa aliwataka Wataalamu wa elimu na Walimu wa shule hiyo kuendelea kuboresha mazingira ya shule hiyo kila fedha inapopatikana pasipo kusahau maeneo ya viwanja vya michezo ambavyo vitawafanya Wanafunzi hao kuburudika na kufurahia masomo.
Aidha aliwashukuru Wahisani na wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa misaada kwa shule hiyo na kuendelea kuwaomba kufanya hivyo kwa kushirikiana na serikali.
Shule ya Wasioona ya Malangali ina jumla ya wanafunzi 92 ambapo 47 kati yao ni wasichana.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa