Mradi wa Shule Bora kwa kupitia shirika la UK Aid wameandaa mafunzo ya Ushirikishaji walimu na Wazazi( UWAWA) pamoja na uongozi wa shule Mkoani Rukwa kwa Maafisa Elimu ya awali na Msingi, Maafisa Taaluma wa Halmashauri , Maafisa Elimu Maalum, Udhibiti Ubora Elimu, Maafisa maendeleo ya Jamii na Maafisa Mawasiliano kutoka Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa.
Lengo la Mafunzo haya ni kuangalia namna jamii itakavyoshiriki kikamilifu kupitia Kamati za Shule ili kuweza kuboresha mbinu za ujifunzaji na ufundishaji katika kuboresha mazingira ya ufaulu Mkoani Rukwa.
Akifungua Mafunzo hayo Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndg. Rashid Mchata amewataka washiriki kutumia mafunzo haya kuhakikisha wazazi wanashirikishwa ili wawe sehemu ya kutatua changamoto za ujifunzaji, ufundishaji na elimu jumuishi ili kuongeza ufaulu, mradi huu utakuwa na manufaa makubwa sana kwa jamii ya Mkoa wa Rukwa
Shule Bora ni mradi wa Serikali unaofadhiliwa na UK Aid . Unatekelezwa katika mikoa Tisa ya Tanzania Bara ambayo ni Rukwa, Mara ,Simiyu, Dodoma, Pwani ,Katavi, Siginda, Kigoma na Tanga kwa ushauri wa kitaalamu kutoka Cmbridge Education ilikishirikana na ADD International, Plan Rescue Committee na Plan International.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa