Anaandika Sammy Kisika.
Waziri wa Wizara ya Maji Jumaa Aweso amewaagiza Meneja wote wa Wakala wa Maji vijijini RUWASA kutumia maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani kwaajili ya kujenga na kuzindua miradi ya maji kwenye maeneo ambayo wananchi bado wanatabika na kero ya maji.
Waziri Aweso aliyasema hayo jana wakati alipokutana na kuzungumza na watumishi wa sekta ya maji pamoja na viongozi wengine mkoani Rukwa.
Aweso alisema haina maana serikali kutoa fedha kwaajili ya ujezni wa miradi ya maji lakini fedha hizo zimekuwa zikakaa pasipo kutumika huku wananchi wakiendelea kuteseka kusaka maji umbali mrefu.
“Nawaagiza nyie Maneja wote kila ifikapo Machi 22, itumieni siku hiyo kwaajili ya uzinduzi wa miradi hiyo na kila wilaya ifanye hivyo, Meneja atakayeshindwa kufanya hivyo ateke maji kwenye ndoo na ajimwagie kichwani kisha aachie ngazi”. Alisema Awesu
Aidha aliwataka Watendaji wa sekta ya maji kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili waweze kutimiza malengo waliyowekewa na serikali na kuacha kutumia muda mwingi kukaa ofisini huku baadhi yao wakiendekeza majungu na uvivu.
Pia aliwataka Maneja wa RUWASA na Mamlaka za maji nchini kuhakikisha wanatenda haki katika kuongoza watumishi wenzao ambao wanawategemea kusimamia maslahi yao.
Alisema..”Kila mtumishi anahitaji kuwa na maisha bora, hivyo watendeeni haki kwa kile kinachopatikana kila mtu apate kulingana na nafasi yake ya kazi”.
Hatahivyo Waziri wa Maji alisema serikali itaendelea kutenga bajeti ya kujenga miradi ya maji kila mwaka ili Wizara hiyo itekeleze mipango yake ya kuwafikishia wananchgi wengi maji kwenye maeneo yao.
Alisema anataka Wizara hiyo iwe Wizara ya maji kweli kweli badala ya kuwa wizara ya ukame kwa mantiki ya kutopeleka maji kwa wananchi huku serikali ya Rais Samia Suluhu ikitoa fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maji.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa