Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimaliwatu Manispaa ya Sumbawanga Kulanga Kanyanga amewataka wananchi wa Manispaa hiyo kuzingatia sheria za usafi ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya taka kwa kila kaya kwa mwezi.
Hayo aliyasema wakati akizungumza na wananchi wa Sumbawanga katika uzinduzi wa Kampeni ya usafi uliofanyika Novemba 25 katika kata ya Mazwi.
Aidha Kanyanga amepongeza jitihada za viongozi wa kata hiyo kwa kuhakikisha kampeni ya usafi inafanikiwa.
Kwa upande wake Mtendaji kata ya Mazwi Sada Kimanta alisema malengo na mipango iliyowekwa ni kuhakikisha mazingira ya kata hiyo yanakuwa safi muda wote huku akitanabaishi Kampeni hiyo inakwenda kwa Kaulimbiu isemayo “Mazwi ng’ara usafi wa mazingira unaanza na mimi na wewe”
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa