Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ameipongeza halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuandaa Mapngo Kabambe wa matumizi ya ardhi ambao unakwenda kuondoa changamoto za migogoro ya ardhi isiyoyalazima.
Dkt.Mabula amesema Mpango huo wa matumizi bora ya ardhi unatakiwakuwa mfano kwa halmashauri zingine hgivyo akizitaka kwenda kuiga Manispaa ya Sumbawanga kwa kuandaa mipango yao ya ardhi.
“Hili sasa natoa agizo kwa halmashauri zote nchini zijifunze kwa Manispaa ya Sumbawanga na ziandae mipango Kabamne kam huu ndani ya mwaka mmoja iwe tayari kwa kila halmashauri”.alisem Dkt.Mabula
Aidha Naibu Waziri huyo amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya kwa kuhakikisha amesimamia mpango huo ambao unaonesha weledi mkubwa kwenye matumizi ya ardhi.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa