Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amewaagiza Wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha wanakamilisha miradi yote ya kimkakati ya Elimu na Afya inayotekelezwa kwenye halmashauri zao kuhakikisha inakamilishwa ndani siku 14 kuanzia hii leo.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa maagizo hayo mara baada ya kukagua miradi hiyo katika Manispaa ya Sumbawanga ikiwapo Shule ya Msingi Sokolo, Shule ya Sekondari Chanji, ujenzi wa hospitali ya wilaya Isofu, Shule ya Msingi Kashai II na nyumba ya Mwalimu ya Shule ya Sekondari Aeshi.
Alisema awali aliaagiza mirado hiyo kukamilisha siku Sita zilizopitakabla ya leo lakini bado haijakamilika licha ya kiuwa ujenzi wake bado unaendelea kwenye maeneo aliyopita.
“Mikoa ya wenzetu kazi ya ujenzi wa madarasa ilishakamilika lakini sisi Rukwa bado, hivyo tunapaswa kukimbizana ili kukamilisha miradi hiyo”alisema.
Hatahivyo ameagiza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo kuende sanjari kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kuyatumia ifikapo Januari mwakani mara shule zitakapofunguliwa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa