Serikali na Wafanyabishara hapa nchini wameshauriwa kuanza kutumia taka zinazozalishwa na binadamu na mimea ili kuweza kuzichakata na kupata nishati ya umeme wa kutosha badala ya kutegemea umeme unaotokana na nguvu ya maji na mafuta pekee.
Ushauri huo umetolewa na Mhandisi wa umeme Bw. Josip Papic wa kampuni ya kigeni ya Afro Bio Energy ya nchini Marekani ambayo inauzoefu wa kuzalisha umeme unaotokana na mimea sanjari kinyesi cha wanyama na binadamu katika nchi mbalimbali duniani, wakati wakizungumza na Madiwa na Watendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Bw. Papic alisema tatizo la uhaba wa nishati ya umeme hapa nchini linaweza kumalizwa kwa kushirikisha wadau kutoka sekta binafsi ambao watazalisha umeme na kuliuzia Shirika la umeme laTANESCO, hivyo kwa kuanza Afro Bio Energy imeonesha nia ya kujenga kiwanda cha kuchakata taka mjini Sumbawanga ambako wakulima na watapatiwa mbegu za nyasi maalumu zitakzozalishwa kwenye mashamba yao na kuiuzia kampuni hiyo ambayo itatumia taka za nyasi hizo na zile zinazozalishwa mjini Sumbawanga kutengeneza umeme wa kiasi cha Megawati 5.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bw. Saad Mtabule alisema ujio wa kampuni hiyo katika Manispaa hiyo na kukamilisha kwa mchakato wa uwekezaji huo utakuwa ni mkombozi kwa uchumi wa halmashauri hiyo na jamii kwa ujumla ambapo ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka zitakazozalisha umeme kinatarajia kutengeneza ajira ya zaidi ya watu Mia tano
Mji wa Sumbawanga unatumia zaidi ya Megawati 5 za umeme kila siku ikiwa ni umeme wa maji kutoka nchi jirani ya Zambia sanjari na umeme wa nishati ya mafuta kutoka mkoani hapa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa