TAARIFA YA IDARA YA MAJI
Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga kupitia Idara ya maji inalo jukumu la kutoa huduma ya maji safi na salama katika eneo la pembezoni mwa mji wa Sumbawanga yaani vijiji vya manispaa, wakati eneo la mjini huduma ya maji hutolewa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SUWASA).
HALI YA HUDUMA YA MAJI KWA SASA
Eneo la pembezoni yaani Sumbawanga vijijini kuna jumla ya kata saba (7) zenye jumla ya vijiji ishirini na tano (25) ambapo kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kwa sasa inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 102,060, ambapo takribani wakazi 51,030 wanapata huduma ya maji safi na salama sawa na asilimia 50 % ya wakazi wote waishio vijijini
JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUTOA HUDUMA YA MAJI
Katika kuhakikisha huduma ya maji vijijini inawafikia wananchi Halmashauri imekuwa ikishirikiana na wadau mbali wa maji kupitia program mbalimbali zikiwemo NORAD, RUDEP, TASAF QUICKWINS, WSDP na RWSSP.
MAFANIKIO
Kuanzia mwaka wa fedha 2012/2013 hadi kufikia Decemba 2017 Halmashauri imekamilisha ujenzi wa miradi mitano kupitia programu ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP) miradi hiyo ni Kanondo, Chelenganya, Mlanda, Malonje na Pito group unao hudumia vijiji vitatu mbavyo ni Pito, Malagano na Tamasenga, kwa ujumla miradi hii inahudumia vijiji saba vyenye jumla ya wakazi 28,657.
UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA
Kwa sasa Halmashauri inaendelea na ujenzi wa miradi mitatu katika vijiji vine yenye thamani ya Tsh 1,948,987,934, miradi hiyo ni Chipu –Kasense, Kisumba –Matanga na Sambulwa –Mtipe, mradi huu unahusisha ujenzi wa tega maji kwenye chanzo cha Sambulwa na bomba kuu toka chanzo cha maji cha Sambulwa hadi Tenki la maji la Mtipe, miradi hii inayoendelea kujegwa itakapo kamilika inatarajiwa kuhudumia wakazi 16,711 hivyo kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama kufikia 67,741 sawa na asilimia 69% ya wakazi wa vijijini.
Miundombinu ya Maji katika Manispaa ya Sumbawanga
AINA YA MIUNDOMBINU
|
HALI YA UPATIKANAJI (VITUO VYA MAJI)
|
||
MAHITAJI
|
ILIYOPO
|
ZIADA/UPUNGUFU
|
|
Maji ya Bomba
|
348
|
174
|
174
|
Chemchem zilizokingwa
|
-
|
7
|
-
|
Visima Virefu
|
-
|
33
|
-
|
Visima Vifupi
|
-
|
0
|
-
|
Uvunaji Maji ya Mvua
|
-
|
5
|
-
|
JUMLA
|
348
|
219
|
174
|
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa