• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Manispaa
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Masuala ya Lishe
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Uratibu na Mipango
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasimali watu
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati na majukumu yake
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi, Elimu & Afya
      • Mipango miji & Mazingira
    • Ratiba za Vikao
      • For Councilors
      • For Hon. Mayor
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
    • Huduma za Kisheria
    • Fedha
  • Kituo cha Habari
    • Albamu ya Picha
    • Video
    • Taarifa Kwa Umma
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Makala
    • Michezo & Burudani

WAKULIMA RUKWA WATAKIWA KUTUMIA ZANA ZA KISASA ZA KILIMO

Ilibandikwa: September 10th, 2019

Na Mwanaidi Waziri

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangambo amewataka wakulima kuachana na kilimo cha mazoea kwa kutumia zana duni za kilimo katika uzalishaji na kujikita katika matumizi ya zana za kisasa ili kuweza kuzalisha mazao    mengi zaidi.

Wito huo wa Mkuu wa mkoa umekuja baada ya kutoridhishwa na mavuno yanayopatikana kila mwaka kwa wakulima mkoani Rukwa licha ya kuwa mkoa huo una maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali.

Alisema hayo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Rukwa kwenye mkutano wa Chama cha Ushirika cha Ufipa Cooperation Union (UCU) kilichofanyika mwanzoni mwa juma kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima.

Wangabo alisema “ni vyema vyama vya ushirika vihimize matumizi ya zana bora za kilimo kwa wakulima kwenye vyama vyote vya Msingi  ili kupanua wigo wa uzalishaji wenye kuleta tija kwa wakulima hao na hata viwanda na uchumi kwa ujumla”

Mkuu huyo wa mkoa alivitaka Vyama hivyo vya Msingi vya wakulima kutumia fursa ya kukopa kutoka kwenye taasisi za kifedha kama vile Benki ya wakulima Tanzania TADB ili kuweza kununua matrekta na hata pembejeo zinginezo.

 Naye Meneja wa Kanda Nyanda za Juu Kusini wa benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Dickson Pangamawe alisema vyama vya Ushirika vya wakulima ni daraja kwao la kupata mikopo hiyo ya pembejeo, elimu na zana za kilimo, hivyo kuwataka wakuli a kujiunga pamoja kulingana na maeneo wanakoishi.

“Wakulima wanatakiwa kuacha kutumia jembe la mkono na kujikita katika matumizi ya matrekta ili kulima maeneo makubwa kwa wakati na kupata matokeo ridhishi na kupunguza upotevu mkubwa wa chakula” alisema

Hata hivyo Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mkoani Rukwa Anyosisye Mbetwa alisema wanataraji kuwasilisha maombi ya mkopo zaidi ya billion 5 kutoka benki ya TADB kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo za kilimo kwenye msimu wa kilimo 2019/20.

Matangazo

  • TANGAZO LA CHANJO KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO April 26, 2023
  • RATIBA YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2023 March 11, 2023
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2023 March 11, 2023
  • TANGAZO LA ZABUNI YA KAZI ZA UBORESHAJI WA BARABARA KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA March 01, 2023
  • Angalia zote

Habari za Karibuni

  • TANGAZO: KUNYANG'ANYWA VIWANJA VYA WANANCHI WALIOCHUKUA VIWANJA NA KUSHINDWA KUVILIPIA KWA MUDA MREFU

    June 30, 2025
  • MKURUGENZI PENDO MANGALI AHIMIZA UADILIFU NA UWABIKAJI KWA WAHITIMU RIBM

    June 20, 2025
  • SHIRIKIANENI NA SERIKALI KULETA MAENDELEO RUKWA-RC MAKONGORO

    March 16, 2025
  • MD PENDO MANGALI-MSIWE MADALALI WA VIWANJA, CHAPENI KAZI

    November 28, 2024
  • Angalia zote

Video

MANISPAA YA SUMBAWANGA KUTAFUTA MZABUNI WA KUZOA TAKA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • History
  • Councilors
  • Photo Gallery

Viunganishi vinavyofanana

  • Public Servant portal
  • Download your Salaryslip here
  • Looking for a job in Public Sector?
  • Get everything from the government
  • Rukwa
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Sumbawanga Municipal Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga

    Simu ya Mezani: +255252802163

    Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255

    Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Uhuru binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa