Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga
Serikali kupitia mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imepata mkopo nafuu kiasi cha Shilingi Billion 55.9 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ulaya (EUROPEAN INVESTMENT BANK – EIB) kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja hiki kwa kiwango cha kimataifa. Na Serikali italipa kiasi cha Tanzania Shilingi Billion 3.3 kwa Wahanga wapatao 97, kutoka Kata zote mbili yaani Kata ya Sumbawanga Asilia wapato 27 na Kata ya Izia 70 na kufikia jumla ya Wahanga 97. Kazi hii itahusisha (Scope) maeneop yafuatayo;
Baada ya ujenzi huu kukamilika utawezesha kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kutumika kwa masaa 24 na kipindi chote cha mwaka.
Ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi walipopita katikati ya Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
Mpango wa Kujenga Kiwanja cha Ndege Eneo la Kisumba
Mkoa umetenga eneo lenye ukubwa wa Hekari 3,411 katika eneo la Kisumba Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege. Eneo hili linamilikiwa na Meneja, Kiwanja cha Ndege Sumbawanga. Matarajio ni kujenga Kiwanja cha Ndege cha kisasa ili kuongeza fursa za usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi. Kwa mujibu wa Meneja wa TANROADS ambaye ana dhamana ya ujenzi na ukarabati wa Viwanja vya Ndege, usanifu (Design) unatarajiwa kuanza Mwaka wa Fedha 2019/2020
Shirika la Posta Tanzania
Utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Shirika la Posta
Ofisi kuu ya Shirika la Posta Mkoa wa Rukwa ipo barabara kuu mtaa wa Mbeya Road, mkabala na Hospital kuu ya Mkoa wa Rukwa, Sumbawanga.
Huduma zinazotolewa na Shirika la Posta Rukwa
Ujenzi wa Barabara za mjini
Barabara ya Majengo - Mashine za Mpunga
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inatekeleza Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mashine za Mpunga – Majengo Min Basi Stendi kwa kiwango cha lami km 2.36. Mradi huu unagharamiwa na fedha kutoka Benki ya Dunia chini ya Mradi wa uboreshaji Miji (ULGSP – Urban Local Government Suport Programme), ambao umefanyiwa usanifu na unasimamiwa na mhandisi mshauri aitwae MUST Consultancy Bureau.
Barabara ya Mpanda – Kanisa la Romani Katoriki Katandala km 2.64
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inatekeleza Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mpanda – Kanisa la Romani Katoriki Katandala km 2.64 njia mbili kwa kiwango cha lami (Asphalt Concrete). Mradi huu unagharamiwa na fedha kutoka Benki ya Dunia chini ya Mradi wa uboreshaji Miji (ULGSP – Urban Local Government Suport Programme, ambao umefanyiwa usanifu na unasimamiwa na Mtaalam mshauri aitwae MUST Consultancy Bureau.
Huduma za Kibenki
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: 0784519681
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa